Tuesday, February 7, 2017

ZANZIBAR HALI TETE KWA WANANCHI

Bado vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu vinaendelea Zanzibar. Leo hii Bwana Kassim Talib ni Dereva wa gari ya Maalim Seif anadaiwa kupigwa na wenye mamlaka amelazwa Hospitali. Tupaze sauti kukemea vitendo hivi.
My Take:
Wahusika wa matendo haya wanajidhihirisha kuwa wao ni kile kizazi halisa cha firauni alie laaniwa. Ila kama labda hawajafahamu ni kwamba watu waovu wanapo kithiri kwa matendo ya uovu huwa wanapewa muda Walau wastaghfiru (watubu) kwa kila aina ya maovu walio yatenda. Kumbe bado inaonekana wanamkataba na "amana" ya UHAI wanaendelea kukithirisha KIBURI na kututhibitishia kuwa wao ni majabari kiasi gani. Kumbukeni Dhulma hizi huja na malipo mabaya sana malipo ambayo mtayapata hapa hapa dunia na akhera hamtabaki salama.
Fahamuni matendo haya hayatojibiwa na raia mnyonge, bali yupo JABARI wa MAJABARI atanyoosha mkono wake na kuyajibu kwa namna ile ambayo anaiona yeye inafaa.
#PumziZinawahadaa

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji