MAJIBU YA CUF KWA LIPUMBA KUTOKANA NA MAHOJIANO ALIYOFANYA LEO KATIKA KIPINDI CHA FUNGUKA KILICHORUSHWA NA AZAM TV (TWO)
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 05/2/2017
Na. Kurugenzi ya Habari –CUF Taifa
MAJIBU YA CUF KWA IBRAHIMU LIPUMBA KUTOKANA NA MAHOJIANO ALIYOFANYA LEO KATIKA KIPINDI CHA FUNGUKA KILICHORUSHWA NA AZAM TV (TWO) AKIHOJIWA NA MKURUGENZI WA KITUO HICHO NDUGU TIDO MUHANDO:
The Civic United front (CUF-Chama Cha Wananchi) kama ilivyowajulisha hapo awali kuwa itatoa taarifa sahihi za Taasisi kwa lengo la kuweka sawa na kuujulisha umma pale patakapotokea upotoshwaji wa masuala mbalimbali yanayohusiana na Chama chetu cha CUF kwa kukusanya taarifa za wiki zima zilizochanya (positive) na au zile hasi (negative) dhidi ya Chama kwa lengo la kuupotosha umma ili wanaChama, viongozi wa Chama, na wananchi kwa ujumla waweze kuwa (updates) na kukaa katika mstari uliosawa kitaarifa. (Weekly CUF information/news review). Leo tarehe 5/2/2017 muda wa saa 3 mpaka saa 4 asubuhi kituo cha luninga cha Azam TV Two kupitia kipindi cha FUNGUKA warusha hewani mahojiano yaliyofanywa kati ya Mkurugenzi wa kituo hicho Ndugu Tido Muhando na Ibrahim Lipumba. Awali napenda kuchukua fursa hii kumpongeza muongozaji wa kipindi hicho ndugu Tido Mhando, mwandishi wa habari nguli wa muda mrefu katika tasnia hii kwa umahiri wake katika uendeshaji wa kipindi pamoja na kuwa na maswali chokonozi (critical questions). Kipindi amekiendesha vyema na kimeweza kumfanya muulizwaji kujibu maswali hayo kwa kujikanganya sana.
Katika mahojiano hayo hakukuwa na jambo jipya lolote kutoka kwa muhojiwa zaidi ya yale yale tuliyowahi kuyasikia kutoka kwake na hasa kwa wale wanaofuatilia masuala ya siasa isipokuwa mambo mawili; Moja Ibrahimu Lipumba ameonyesha kutokujua jinsi ya muundo wa Muungano wa Mkataba unavyokuwa na suala la pili ni kwa mara ya kwanza tangu wizi wa fedha za Ruzuku kufanyika tarehe 5 January, 2017 leo amejitokeza hadharani na kujaribu kueleza jinsi walivyofanya wizi huo wa kuchepusha shilingi 369 milioni kinyume na katiba na taratibu za Chama. Masuala hayo na mengine yatafafanuliwa katika taarifa hii kwa mukhtasari. Tulichojifunza ni kwamba Ibrahimu Lipumba amepoteza uwezo na nguvu ya kujenga hoja, lakini pia amepoteza muelekeo wa kisiasa na kumsababisha kujitia msongo wa mawazo ambao kama angekubaliana na ushauri aliopatiwa hapo awali asingeweza kufika hapa alipojifikisha. Amepoteza heshima aliyojijengea kwa watanzania, wanaCUF na watanzania wengi wapenda mabadiliko nchini. Aidha yapo machache ambayo ameyaeleza vizuri na kwa usahihi.
Kwa mukhtasari tunapenda kufanya majumuisho na kujibu hoja alizozitoa kwa upotoshwaji na au kutokujua kama ifuatavyo:
1. Kuhusu Muungano wa Mkataba;
Lipumba ameeleza kuwa afahamu nini maana ya Muungano wa Mkataba na muundo wake jinsi ulivyo? Na kwamba alitofautiana na Chama kuhusu suala hilo. Hili si suala geni limeelezwa kwa kirefu sana na wasomi waliobobea katika fani ya sheria na kufanyiwa uchambuzi na waandishi kadhaa wa habari kwa kuandikia makala za kuelezea dhana sahihi ya Muungano wa Mkataba. Ni ukweli kuwa CUF kwa wakati uliopita ulikuwa unaamini juu ya sera ya muundo wa Muungano wa serikali tatu. Lakini sera ni muongozo tu wa jinsi ya suala husika makhsusi namna linavyotakiwa kushughulikiwa. Sera inaweza kubadilika kulingana na haja, wakati, na malengo husika yanayokusudiwa kufikiwa kwa dhamira njema. Wazanzibari kwa ujumla wao bila ya kujali itikadi ya vyama ukiondoa wahafidhina wachache wanaonufaika na mfumo uliopo sasa, wanadai mamlaka kamili ya nchi yao. Mamlaka kamili ya nchi yao yatapatika kwa kuwa na Muungano ulioundwa katika mfumo sahihi. Treat based union (Muungano wa mkataba) ni njia sahihi ya kulinda mamlaka kamili ya nchi ya Zanzibar. Jaji Mstaafu wa mahakama kuu Mheshimiwa Abubakari Khamisi aliwahi kuwasilisha mada kamili chini ya uenyekiti wa Ibrahimu Lipumba wakati huo pale katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam tarehe 23 Disemba mwaka 2013. Hakuna mzanzibar anayekataa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Inasikitisha lakini haishangazi sana kwa kuwa Lipumba ni msomi wa fani ya uchumi na si sheria. Hata hivyo kama una nia njema kwa kupitia maandiko ya jambo husika kwa usomi wa mtu alionao hata kwa fani tofauti unamfanya muhusika kuwa na uelewa wa haraka ya nini kinachokusudiwa na ukapata mantiki ya hoja zinazoelezwa.
Muungano wa kikatiba kama huu uliopo sasa wa mwaka 1964 ulioasisiwa na msingi wa Mkataba wa Muungano (Articles of Union) una athari kubwa kwa pande zote mbili na hasa kwa Zanzibar kwa udogo wake na kwa kupoteza mamlaka yake ya asili. Unapozungumzia Muungano wa mkataba (Treat based Union) unakusudia mahusiano yatakayojengwa kwa kuirejeshea Tanganyika na pia Zanzibar mamlaka yao kamili ya kidola na yatawezesha kuwapo na utaratibu wa ushirikiano kati ya nchi mbili zilizo sawa na zilizo huru na zenye mamlaka kamili ya kidola. Mkataba utaoongoza mahusiano hayo utaweka wazi A-Z ni mambo gani nchi hizo zitashirikiana na namna ushirikiano wao utavyopaswa kuwa. Pale nchi iliyo na mamlaka yake kamili inapoandikiana mkataba wa kuwa na ushirikiano au muungano na nchi nyingine inakuwa haiyapotezi mamlaka yake au uhuru wake. Hali hiyo ni kinyume na Muungano wa kikatiba uliopo sasa ambao umeifanya Zanzibar iyahaulishe kwenye Serikali ya Muungano mamlaka na madaraka yake ya kimsingi. Zanzibar imezitoa mhanga nguvu zake za kidola wakati mwenzake Tanganyika haikulazimika kujitosa na kutoa mhanga kama huo kwa vile utawala wa Tanganyika unaendeshwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Tunamtaka Lipumba na wenzake wanaofanana kifikra wafahamu kuwa ushirikiano au muungano wa Mkataba ni kwamba kila nchi iliyotia saini mkataba wa muungano inakuwa na nguvu ya ‘turufu’. Hivyo hata katika mambo yaliyokubaliwa kuingizwa katika ushirikiano nchi inayohusika inaweza kuitumia nguvu yake ya turufu na ikaomba hifadhi ya watu wake endapo inahisi kwamba inahatarishwa na sera za huo muungano katika utekelezaji wa mahusiano na ushirikiano wa nchi hizo. Muungano wa aina hiyo, yaani wa Mkataba, utairejeshea Serikali ya Umoja wa Kitaifa mamlaka na madaraka muhimu ambayo Zanzibar haikuwa nayo kwa muda wa miaka 52 sasa. Yakitumiwa vyema madaraka hayo yataiwezesha Zanzibar kutekeleza sera zitazoirejeshea Zanzibar adhama na fahari iliyokuwa nayo zamani na kuifanya ishiriki kikamilifu katika shughuli za kanda ya Afrika ya Mashariki na ya Kati na kupindukia mipaka ya kanda hii.
Athari za Muuungano wa Kikatiba tuliona hivi sasa:
• Miaka 50 ya Muungano haikuinufaisha Zanzibar inavyostahiki kiuchumi, kisiasa, kiusalama, na kijamii.
• Muungano umeifanya Zanzibar itoweke kwenye ramani ya dunia.
• Muungano umeifanya Zanzibar idhurike kisiasa, kiuchumi na kijamii ikilinganishwa na visiwa vingine kama vile Mauritius na Seychelles.
• Muungano umesababisha dhiki za kiuchumi na shida za kijamii zinazoisibu Zanzibar kwa muda wa takriban nusu karne.
• Muungano umewadhalilisha na kuwaondolea amani na utulivu wa kisiasa wazanzibari na kusababisha maafa makubwa hasa kila unapofanyika uchaguzi ambao unasimamiwa na vyombo vya dola vya Muungano/Tanganyika.
• Muungano umeiondolea Zanzabar Hadhi na heshima yake kitaifa na kimataifa.
• Muungano umeifanya Zanzibar kushindwa kujiamulia njia ya kiuchumi na kijamii ya kuifuata ili iweze kujikomboa kutokana na mateso, shida na dhiki ilizo nazo.
• Muda wa miaka 50 serikali ya Muungano haikuyatumia vyema madaraka iliyoyatwaa kutoka Zanzibar kupigana na adui ujinga, maradhi, ubadhilifu, matumizi mabaya ya madaraka na umasikini.
• Muungano wa kikatiba hautoi fursa/nafasi kwa njia nafuu ya kuufanyia marekebisho kila inapobidi kufanya hivyo ikilinganishwa na Muungano wa Mkataba.
Kwa mukhtasari huu ndio Muungano wa Mkataba. Na faida zake ni kinyume na athari tulizozieleza katika nukta 9 hapo juu. Lipumba anapaswa kufahamu kuwa kwa vyovyote iwavyo mapambano ya wazanzibari na watanganyika madhubuti walio makini katika kudai haki na usawa katika Muungano wetu hayatarejeshwa nyuma.
2. Kuhusu UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI-UKAWA;
KWA bahati njema sana katiba ya CUF haitoi nafasi kwa masuala makubwa kuamuliwa na mtu au kiongozi mmoja kama zilivyo katiba ya vyama vingine. Mathalan vyama vingine Katibu Mkuu wa Chama anateuliwa na Mwenyekiti wa Chama pekee. Ndani ya CUF hilo na mfano wa hayo halipo. Lazima masuala yapitie ndani ya vikao vya maamuzi na vina mamlaka ya kukubali au kukataa pendekezo lolote litakalowasilishwa katika kikao husika na kiongozi yeyote yule aliyepewa mamlaka ya uteuzi. Suala la mashirikiano ya vyama si jambo geni nchini iwe katika msuala ya ajenda mahususi au wakati wa uchaguzi. Mwaka 2000 CHADEMA haikusimamisha mgombea urais, chini ya uenyekiti wa Mzee Mtei na Katibu wake marehemu Bob Makani walimuunga mkono mgombea wa CUF wa urais(ambaye alikuwa yeye Lipumba). UKAWA uliasisiwa na Ibrahimu Lipumba na wenzake wakiwa katika bunge la katiba
Sunday, February 5, 2017
FUNGUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI
Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri
-
Ili kuweza kuweza kumlainisha mpenzi wako chumbani ni lazima umnyenyeke yeye kama yeye na maneno malaini kama..,...............................
No comments:
Post a Comment