Sunday, March 13, 2016

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameamuru vikwazo kuwekelewa dhidi ya safari za nchi za nje

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameamuru vikwazo kuwekelewa dhidi ya safari za nchi za nje na maafisa wa serikali kama njia ya kupunguza gharama ya kuendesha serikali.
Akihutubia kongamano la kila mwaka la uongozi katika mji wa Gabiro, mashariki mwa nchi, Kagame alisema kuwa safari zisizofaa za nchi ya nje zimekuwa zikitumika na maafisa wa serikali kupoteza wakati na raslimali ya serikali.
Kagame alisema anakubaliana na rais wa Tanzania John Magufuli ambaye alichukua hatua kama hiyo ya kupiga marufuku safari zisizofaa na watumishi wa umma. Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na viongozi 250 lilijadili mbinu mbali mbali za kuleta mageuzi ya kijamii nchini humo na mipango ya maendeleo katika miaka zijazo.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji