Tuesday, February 7, 2017

USIKOSE KUSOMA HAPA

HATA AIBU HAYANA HAYA MAJITU
SIMON SIRO: TUMEMKAMATA MH. TUNDU LISSU KWA MANENO YA UCHOCHEZI KUHUSU UWEPO WA NJAA
Mbunge wa Singida Mashariki anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi kuhusu kuwepo kwa njaa nchini.
Hatua hiyo inafuatiwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kupinga kuwepo kwa njaa nchini na kwamba, wafanyabiashara wachache wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya watu kueneza taarifa hizo.
Simon Siro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam leo amewaambia waandishi wa habari kwamba, wanamshikilia Lissu kutokana na tuhuma hizo.
Si mara ya kwanza Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukamatwa kwa madai yanayofanana na hayo.
Miongoni mwayo ni tarehe 22 Desemba mwaka jana ambapo Lissu aliachwa baada ya saa kadhaa kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kutumia jina la Rais Magufuli kwa dhihaka kwa kumwita rais mtukufu.
Alianza kuulizwa kuhusu mkutano wake na waandishi wa habari alipozungumzia kupotea kwa Ben Saanane, aliyekuwa msaidizi wa karibu wa Mbowe “aliitwa kuhojiwa juu ya Press conference aliyofanya na kuzungumzia suala la Saanane lakini pia wamemuhoji anamaanisha nini kumwita Rais John Magufuli jina la “Mtukufu.”
Lissu alikamatwa jana jioni mjini Dodoma katika vianja vya bunge na kusafirisha moja kwa moja hadi jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukamatwa kwake, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa alieleza kutojua sababu za kukamatwa kwake.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa, Lissu anaendelea kuhojiwa kutokana na tuhuma hizo.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji