Katika matangazo yetu jioni hii: Mkutano wa Baraza la Haki za Binaadamu umefunguliwa leo mjini Geneva Uswisi. Mada kuu zinazotazamiwa kujadiliwa ni uvunjwaji wa haki za binaadamu katika sehemu tofauti za dunia. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guteres amekuwa mtu wa kwanza kuhutubia mkutano huo na ameelezea wasi wasi wake juu ya kuchipuka kwa hisia za uzalendo wa siasa kali.
No comments:
Post a Comment