Friday, February 10, 2017

Du huyu jamaa kiboko

Nakumbuka kipindi najiunga na Facebook nilimuadd Mdada mmoja hivi mzuri balaa yani ukicheki picha zake lazima udate
Kipindi hicho nilikuwa sijaweka picha hata moja sababu simu ambayo nlikuwa natumia camera yake ilikuwa mbovu nilivyomuadd huyo mdada nikamfuata inbox maongezi yakawa hivi
RAPHAEL.........mrembo mambo vipi??
MREMBO..........poa tu Raphael
RAPHAEL.......pande zipi mrembo??
MREMBO...........mimi naishi bara bara 8 jiran na (M THE BEST) sijui ww mwenzangu
RAPHAEL......mimi naishi Mwaisen karibu sana
MREMBO........asante sana wangu huko Mwaiseni ni nyumbani kwenu au nyumbani kwako????
RAPHAEL......haha acha hizo bhana mimi mtu mzima nina maisha yangu huku naishi kwangu nina mjengo nimeununua mwaka jana
MREMBO.......mmh unaishi na nani umeoa??
RAPHAEL......hapana bado sijaoa bt nataka mwaka huu nitafute mchumba sababu nimeshakuwa tajiri biashara nyingi zinanibana nataka ntafute mke tuwe tunasaidiana
MREMBO........mmh jmn mbona wachumba tupo wengi plzzz ntumie namba yako tuongee nikuambie kitu
Mrembo alivyoomba namba yangu nikamtumia mda huo huo akanipigia maongezi yakawa hivi
MREMBO......Raphael mpenzi hivi ni kweli unatafuta mchumba???
RAPHAEL.....yaah natafuta coz wazazi wangu ni watu wenye pesa nyingi sana mimi pia nshakuwa tajiri sasa kwann nisitafute mwanamke wa kutumia nae hizi pesa zangu
MREMBO.....kwani mda huu ukwapi natamani sana nkuone
RAPHAEL.........mda huu nipo hapa Chanji sokoni kuna vitu nimekuja kuangalia nataka niwanunulie watoto yatima nikawape msaada kwenye vituo vyao
MREMBO......woow basi nisubiri hapo hapo nachukua Bajaji nakuja ili twende wote huko kutoa msaada my love plzz nsubiri hadi nije
RAPHAEL.......ok mrembo fanya fasta basi nakusubiri ukifika nijulishe
Nilivyomjibu hivyo Mrembo akakata simu nilikaa kama dakika 45 nikasikia simu yangu inaita nikacheki nikaona ni huyo mrembo ananipigia nikapokea maongezi yakawa hivi
MREMBO.......RAPHAEL nimeshafika Mwaisen hapa upo sehemu gani
RAPHAEL.......nipo hapa sokoni karibu na wanapouza mikungu ya ndizi
MREMBO.....mbona hata mimi nipo hapa hapa nielekeze sehemu uliyopo
RAPHAEL.....umevaaje??
MREMBO.....kigauni chekundu kifupi na viatu virefu nimebeba pochi ya bluu
RAPHAEL.........okey nishakuona angalia mbele yako si unaona kuna mtu anachoma Mahindi amevaa pensi ya chadema na tisheti ya dume condom chini amevaa chachacha ndo mimi RAPHAEL MBALAMWEZI niliyekuita njoo basi ule hata muhundi bby
Nilivyomjibu tu hivyo akakata simu nikamuona anaita Bodaboda akasepa mimi nikabaki nacheka tu na wauza mahindi wenzangu nikapiga tena namba yake nikakuta kanifungia nikaingia Facebook nikakuta kanipiga block dah
Mabint mungu anawaona mjue kwan ss tusio na kitu sio watu

No comments:

ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI

Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri