Malaika wawili walikuwa wakisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ilipofika jioni, wakaingia katika nyumba ya mzee tajiri kwa ajili ya kulala. Usiku ulipofika, mzee yule tajiri hakutaka walale katika nyumba yake ya kifahari, hivyo akawapa chumba kimoja kikuu kuu, kilichokuwa na baridi na tena huku akiwa amewaambia walale sakafuni.
Wakati wameweka godoro lao usiku kwa ajili ya kulala, malaika mmoja akaona tundu katika ukuta, akainuka, akalifuata tundu lile na kisha kuliziba. Kitendo kile kikamfanya yule malaika mdogo kuuliza kwa nini alifanya vile. Malaika yule akajibu 'MARA KWA MARA VITU HAVIONEKANI KAMA VINAVYOONEKANA'.
Siku iliyofuata malaika wale wakaendelea na safari yao na kulala usiku katika nyumba ya masikini mmoja ambaye alikuwa akiishi na mke wake. Katika nyumba ile, walipewa chakula japokuwa hakikuwa kingi, walipewa sehemu nzuri ya kulala japo haikuwa kubwa, walifanyiwa ukarimu mkubwa.
Walipoamka asubuhi, mzee yule masikini pamoja na mkewe walikuwa wakilia kwa sababu ng'ombe wao ambaye walikuwa wakimtegemea kwa kuwagawia maziwa alikuwa amekufa asubuhi hiyo. Hapo ndipo malaika yule mdogo akauliza:
"Kwa nini umeruhusu hili kutokea? Kwa yule mzee tajiri ambaye alikuwa mchoyo wa kutufanyia vitu kadhaa ulimsaidi kwa kumzibia tundu lililokuwa ukutani ila kwa huyu mtu masikini ambaye ametupa kila tulichohitaji umeruhusu ng'ombe wake anayemtegemea kufa?"
Malaika yule mkubwa akajibu "Jana tulipokuwa kwa yule mzee tajiri, pale ukutani niliiona dhahabu akiwa ameichimbia, nilichokifanya ni kuliziba lile shimo ili ile dhahabu isionekane tena. Usiku wa jana tulipokuwa tumelala, malaika wa kifo alifika mahali hapa kwa kuwa alitaka kumuua mke wa masikini huyu, nilichokifanya, nikamwamuru amuue ng'ombe badala ya mke wa mzee huyu'
Naomba uniambie unajifunza nini kutokana na simulizi hii.
Saturday, February 11, 2017
CHUKUA SEKUNDE KADHAA KUSOMA HAPA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI
Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri
-
Ili kuweza kuweza kumlainisha mpenzi wako chumbani ni lazima umnyenyeke yeye kama yeye na maneno malaini kama..,...............................
No comments:
Post a Comment