Tuesday, March 15, 2016

Waasi wa Sudan People's Liberation Movement (SPLM),

Waasi wa Sudan People's Liberation Movement (SPLM), nchini Sudan, wamedai kuua wanajeshi 40 wa serikali na kujeruhi wengine 80 katika eneo la Jebel Kalgo, yamkini kilomita 30 kutoka mji wa Al-Damazin, ndani ya jimbo la Blue Nile.
“Wapiganaji wetu walitibua jaribio la pili la uvamizi na wanajeshi wa serikali katika kipindi cha wiki moja,” Arno Taloudy, msemaji wa kundi hilo alisema. “Tuliua wanajeshi 40 na kujeruhi wengine 80 huku wapiganaji wetu wawili wakiuawa na watatu wakipata majeraha,” alisema. Hata hivyo upande wa jeshi haujatoa taarifa kuhusiana na tukio hilo.
Jimbo la Blue Nile limeshuhudia mapigano tangu mwaka wa 2011 kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa SPLM.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji