Tuesday, March 15, 2016

pemba watu wahama kwa kukimbia makaaziyao

hama cha Wananchi (CUF) kimedai kwamba baadhi ya wanachama wake kisiwani Pemba wameanza kukimbilia msituni kutafuta upenyo wa kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Kenya.
Chama hicho kimedai kuwa wananchi hao wanakimbia operesheni za kamatakamata zinazoendelea ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Machi 20, mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma, Hamad Masoud Hamad, alidai kuwa tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka 2015, kumekuwapo na uingizwaji wa askari, vifaa na zana nzito za kivita katika visiwa vya Unguja na Pemba sambamba na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaoranda randa mitaani wakiwa na silaha za kivita.
“Sasa hivi kuna taharuki kubwa sana Pemba kutokana na vyombo vya ulinzi vilivyovamia na kuikalia Pemba na kuna makumi ya watu sasa hivi wapo maporini na wanaangalia uwezekano wa kutoroka Pemba kukimbilia Mombasa nchini Kenya. Hii inatokana na Pemba kuonekana imekaliwa kijeshi. Watu watadhalilishwa, wataumizwa, watapigwa, wanavyofikiria wao tusije tukashangaa nusu ya watu wa Pemba wakajikuta wapo huko Mombasa, Kenya,” alidai Hamad, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji