\Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mkuu wa Polisi wilaya
ya Arusha MrakibuwaPolisi (SP) Jumanne Muliro amevitaka vikundi vya
ulinzi shirikishi pindi wanapokuwa katika kazi za doria kutowabughudhi
wananchi badala yake wanatakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria.
Alisema utendaji bora
wa kazi kwa kuzingatia nidhamu na sheria utaongeza imani kwa wananchi
hali ambayo itawafanya wajitolee na kuendelea kuvichangia vikundi hivyo
hatimaye kuboresha maslahi yao wenyewe na vikundi hivyo kwa ujumla kwa
maana ya vifaa.
“Hakuna
sheria inayomkataza mtu yoyote kutembea usiku lakini pia ni jukumu lenu
nyinyi askari kumhoji yeyote mtakayekutana naye usiku kwa kutumia
taaluma mlionayo nayo ili kuweza kubaini ukweli” Alifafanua Mkuu huyo wa
Polisi.
No comments:
Post a Comment