Wednesday, August 23, 2017

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba wa ufungaji wa mitambo

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba wa ufungaji wa mitambo minne ya Rada ya kuongozea ndege baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales Air System ya nchini Ufaransa. Hafla hiyo pia imeambatana na uzinduzi wa nembo ya mpya ya TCAA leo jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti Bodi ya TCAA, Prof. Longinus Rutasitara, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System, Bwana Abel Curr. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(wapili kushoto aliyesimama), akishuhudia utiaji wa saini ya mkataba wa ufungaji wa mitambo minne ya Rada ya kuongozea ndege baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari (Kushoto) na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System ya nchini Ufaransa, Abel Curr .wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeingia makubaliano ya manunuzi ya rada Nne na kampuni ya Thales ya nchini Ufaransa zenye thamani ya sh.bilioni 61.3.
Akizungumza leo na waandishi wa habari kabla ya kusaini makubaliano ya manunuzi ya rada hizo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema kuwa kampuni hiyo ifunge kwa viwango vilivyoainishwa katika mkataba na watakaosimamia mradi huo wanatakiwa kuwa na uadilifu kutokana fedha hiyo ni nyingi kutolewa na serikali.
Amesema kuwa kufungwa kwa rada hizo kutasaidia serikali kupata mapato ya sh. bilioni moja, kuongeza idadi ya ndege kutumia anga ya Tanzania pamoja na kuongeza idadi ya wataalii kutokana na anga kuwa salama.
Profesa Mbarawa amesema kuwa TCAA imetumia fedha zake pamoja na serikali kuepukana na mkopo ambapo wameweza kuokoa sh. bilioni 10 ambazo zingetokana ulipaji mkopo katika taasisi ya fedha.
Amesema kuwa TCAA wameweza kujibana hadi kufikia ununuzi wa rada hizo na kutaka taasisi zilizo chini ya wizara kutumia vyanzo mapato vyao katika miradi mbalimbali kuliko kuangalia kukopa katika taasisi fedha benki.
Nae, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johar amesema kuwa rada hizo zitafungwa katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam , Kilimanjaro, Songwe -Mbeya pamoja na Mwanza.
Amesema kuwa TCAA kwa kufungwa rada hizo inakwenda kimataifa kutokana na huduma zinazotolewa na mamlaka hizo kuzingatia viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).
Aidha amesema kuwa rada hizo ni matokeo ya serikali ya awamu ya tano katika kufikia uchumi wa kati kufikia 2025 unaoendana na pamoja na usafiri wa anga.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa TCAA, Profesa Longinus Rutasitara amesema kuwa TCAA imejibana katika vyanzo vyake na kuweza kununua rada hizo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa( katikati), akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari (Kushoto) na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System Abel Curr wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini ya mkataba wa ununuzi wa rada nne za kuongozea ndege. wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA huku akishuhudiwa na makamu Mwenyekiti Bodi ya TCCA, Prof. Longinus Rutasitara,(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza S. Johari.(kushoto) wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba wa ufungaji wa mitambo minne ya Rada ya kuongozea ndege baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales Air System ya nchini Ufaransa leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza S. Johari. (Kushoto) wakishangilia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA, wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba wa ufungaji wa mitambo minne ya Rada ya kuongozea ndege baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales Air System ya nchini Ufaransa leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI

Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri