wanne wapya wakila Kiapo cha Uaminifu.
Wabunge hao ni wale walioteuliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Mbunge mmoja aliyechaguliwa baada ya Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017.
Wabunge hao ni pamoja na Mhe. Alhaji Abdallah Majura Bulembo, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Mhe. Anne Kilango Malecela na Mhe. Ali Juma Ali -
(Jimbo la Dimani).
Mkutano huu wa sita ambao umeanza Jumanne tarehe 31 Januari 2017 na unatarajia kumalizika tarehe 10 Februari 2017 utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni.
Aidha, katika kikao cha kwanza cha Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zimewashilishwa na Mawaziri kuhusu;
Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.
Katika Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika mwezi Novemba, 2016 Miswada mitatu (3) ya Sheria ilisomwa kwa mara ya Kwanza Bungeni na kupelekwa kwenye Kamati husika iliifanyiwe kazi.
Hivyo katika Mkutano huu wa Sita Miswada hiyo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mara ya Pili, kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 91. Miswada hiyo ni:-
(i) Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).
(ii) Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).
(iii) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)
Saturday, February 11, 2017
Ukikosa tv pitia hapa shuli za bunge
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI
Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri
-
Ili kuweza kuweza kumlainisha mpenzi wako chumbani ni lazima umnyenyeke yeye kama yeye na maneno malaini kama..,...............................
No comments:
Post a Comment