Wednesday, March 9, 2016

Serikali ya mkoa wa Tibet nchini China imetenga dola milioni 75

Serikali ya mkoa wa Tibet nchini China imetenga dola milioni 75 zitakazotumika katika kipindi cha miaka mitano zijazo kukarabati na kulinda “makaburi ya angani”.
“Makaburi ya angani’ ni aina ya mazishi maarufu katika utamadumi wa wenyeji wa Tibet ambapo wafu hulishwa kwa ndege wala wanyama ili roho zao zifike mbiguni. Takriban maeneo 156 ya “makaburi ya angani’ yatanufaika na fedha hizo.
Taka zinazotokana na shughuli za mazishi, mbwa mwitu, barabara mbaya na ukosefu wa miundombinu muhimu zimeathiri pakubwa utamaduni huo. Fedha hizo zitagharamia ujenzi wa barabara, vyumba vya mapokezi, vyumba vya kuhifadhia maiti na vyumba vya kuchomea taka.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji