Wednesday, March 9, 2016

Kwali akili ni nwyele kila mtu ana zake

Maziwa ya mbuzi yaliyokuzwa kisayansi, au GMO, yanaweza kutumika kutengeneza madawa ya bei nafuu ya kutibu ugonjwa wa saratani, wanasayansi kutoka New Zealand wamesema.
Wanasayansi hao wa chuo kikuu cha Auckland wamedhibitisha kuwa maziwa ya mbuzi yaliyokuzwa kisayansi yana kiungo muhimu aina ya “mono-clonal antibodies” (MCA) ambacho hutumika kutengeneza madawa ya kutibu saratani.
Wanasayansi hao wamesema kuwa kiungo hicho kinasababisha seli za mwili zilizoathiriwa na saratani kuonekana kwa urahisi ili kurahisisha matibabu na pia zinafanya seli hizo kudumaa na kutoenea mwilini.
Wamesema kuwa uzalishaji wa madawa hayo hautakuwa na gharama ya juu na hivyo basi bei zao zitakuwa nafuu ikilinganishwa na bei ya madawa za saratani za sasa. New Zealand inaongoza duniani kwa ufugaji wa mifugo na uzalishaji wa maziwa.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji