Sunday, March 6, 2016

JAMII IJITOKEZE KUSAIDIA

Jamii ijitokeze kuwasaidia wasiokuwa na uwezo -Kaiza
Jamii ya watu wenye uwezo wa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwasaidia myatima na watoto wasiojiweza ili kuendeleza maisha yao ya kila siku.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Chake chake Mkoa wa kusini Pemba Mh.Yussuf Kaiza Makame wakati akikabidhi msaada wa chakula kwa mayatima na watoto wasiojiweza eneo la madungu jimboni humo.
Kaiza alisema ni jambo la msingi iwapo wananchi wenye uwezo watajitokeza kwa wingi kuwasaidia wasiokuwa na uwezo kutokana na hali ngumu ya maisha ni sawa na kuwaendeleza watoto hao katika maisha yao ya kila siku.
Alieleza kuwa uwepo wa hali ya utofauti wa kimaisha kwa jamii ni jambo la kawaida na haliwezi kuepukika hivo ipo haja kwa wenye uwezo kuwasaida wengine wasiokuwa na uwezo.
‘’Kusaidiana kunaleta umoja na upendo katika jamii hivo kuna kila sababu watu wa aina hii kusaidiwa ili kuhisi faraja’’alisema Kaiza.
Alieleza kuwa licha ya kuwasaidia watoto hao chakula lakini kuna haja ya kuelekeza zaidi katika suala la elimu kwani ndio msaada muhimu kwa watoto hao katika maisha yao ya badae.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya watoto hao na familia zao wameleza kufarijika sana na msaada huo huku wakitoa wito kwa jamii na taasisi mbali mbali kuelekeza ngvu zao kwa watu wasiojiweza.
Walisema jambo analofanya Mbunge huyo kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali katika suala la maendeleo ni la kuigwa na kupigiwa mfano na wengine wote.
Takribani watoto zaidi ya 70 jimboni humo wamepatiwa msaada wa chakula ili kuweza kukidhi mahitaji yao.

No comments:

ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI

Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri