Tuesday, March 15, 2016

CUF YATAKA USALAMA WA WANANCHI WAKATI WA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR.

CUF YATAKA USALAMA WA WANANCHI WAKATI WA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR.
Kuelekea uchaguzi mkuu wa marudio Zanzibar chama cha upinzani cha CUF ambacho kimetangaza kutoshiriki uchaguzi huo kimevisihi vyombo vya ulinzi na usalama kusimamia amani kwa sheria na katiba ili kunusuru wakimbizi wa siasa kutokana na hofu kubwa iliyotanda kisiwani pemba ambapo baadhi ya watu wako Mafichoni.
Msimamo huo umetolewa na kaimu mkurugenzi wa habari,ueneiz na mawasilaino kwa Umma Bw.Hamad Masoud wakti akiongea na wandishi wa habari ambapo amesemea hali kiswani Pemba sasa si shwari huku wanchi wakinyimwa fursa zao za haki za binaadamu ambapo hivi sasa watu hawaruhusiwi kuwepo mitaani ikifika saa mbili usiku na baadhi ya watu wamekimbia makazi yao.
Aidha chama hicho kimevisihi vyombo vya ulinzi na usalama kuacha kuegemea upande mmoja na kutekeleza wajibu wao kwa misingi ya sheria na katiba huku chama hicho kikishtushwa na ujio na uingwizaji mkubwa wa askari na magari na zana nzito za kivita hivyo CUF imetaka amani isimamaiwe kwa wote.
Kukiwa kumebakia siku sita kufanyika uchaguzi huo wa machi 20 kwa upande wa unguja hali ianendelea kuwa shwari na wanachi kuendelea na shugulki zao kama akwaida huku mazungumzo makubwa ya mitaa mbali mbali na suala la uchaguzi huo wa jumapili.

No comments:

SIKU YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VIJANA

Mkuu wa wilaya amewataka v ijana kuweza kupa mbana na o vitendo vya Uzalilishaji