Wednesday, March 9, 2016

CCM ZANZIBAR INAPOOGOPA KIVULI CHA SEIF SHARIF HAMAD

"Kama ilivyo kawaida kwa viongozi mbalimbali kutembelea wenzao wanapokuwa hospitali, jana ilikuwa tofauti kwa Maalim Seif baada ya klutoonekana kwa kiongozi yeyote kutoka Serikali ya Zanzibar wala ya muun gano" ( Gazeti Mwananchi la leo limeripoti)
Kisa hiki kinanikumbusha kisa kilicho shabihiana cha Firauni(Pharoh) na Nabii Mussa (Moses). Wakati Moses ilipogundulika kuwa ni myahudi na si mwana familia ya Firauni, na kwamba anatyarisha mipango ya kuwakomboa wana waisrel kutoka utumwani( out of bondage), Firauni ilimlazimu kutowa fatwa ya kupiga marufuku kusikika, kutajwa au hata kukumbukwa jina la Moses katika himaya yake
Tukiangalia uhasama huu wa kijinga na kishenzi umetokana na nini hasa? ni kutokana na siasa, kugombania ulwa au kujishuku tu? Ni ujinga hasa kwa sisi wazanzibari ambao mara zote tunapenda kujitofautisha na wengine kwa kujifanya ni waungwana, wastaarabu na wenye kuhurumiana.
Kama Firauni ilimlazimu kutowa fatwa ya kupiga marufuku kusikika, kutajwa au hata kukumbukwa jina la Moses ndivyo vyombo vya habari vya taifa( hasa Zanzibar), ZBC na gazeti la Zanzibar Leo vyote kwa pamoja vimelemazwa kuwa na ububu, uziwi na upofu kwa kufuata fatwa hiyo dhidi ya Maalim Seif.
Raisi John Pombe Magufuli amefika Serena Hotel - Dar Es Salaam, kwa ajili ya kumjuulia hali, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alipata ruhusa jana baada ya kulazwa kwa siku moja katika hospitali ya Hindu Mandal, jijjni Dar es Salaam, baada ya kujisikia vibaya ghafla alipowasili Julius Nyerere International Airport, Dar Es Salaam, Tanzania!
Kipi hapa kinachotisha ni nini hasa; ni Maalim Seif au kivuli chake?

No comments:

ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI

Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri