Monday, November 16, 2015

LOWASSA ATOWA SIFA

Baada ya kutoa sifa nyingi kwa raisi wetu kwa kufanya ziara za kushtukiza pale muhimbili ambazo ni kama zimezaa matunda kwa kipimo cha MRI kuanza kufanya kazi, hebu sasa na tujiulize juu ya viapaumbele vya serikali yetu kama vipo sawa.
Hebu tuangalie kuhusu vipimo hivi viwili vya ct scanner na mri. Kwa mujibu wa wizara ya afya vipimo hivi vilisuswa kufanyiwa matengenezo baada ya kampuni ya Phillips kutolipwa deni lake kuvifanyia ukarabati vipimo hivyo ambalo limefikia bil. 7. Na juzi wamelipwa bil. 3 ndio kikafanyiwa matengenezo. Kwa maana hiyo serikali bado inadaiwa bil.4.
Tanzania tunavipimo hivyi katika hospitali moja tu ya muhimbili kati ya hospitali zote za serikali hapa nchini, hiki ni kichekesho na tena ni aibu!
Kwa mujibu wa kampuni ya Phillips, moja ya makampuni yanayotengeza hivi vipimo, bei ya hivi vipimo ni kati ya USD 150,000 - 250,000 yaani sh. Mil 300 _ 500 za kitanzania kwa ct scanner ya slice 16 na USD 250,000 - 300,000 yaani Tsh. Mil. 500 - mil 600. Kwa ct scanner ya slice 64. Na gharama za kuifunga pamoja na mafunzo ni tsh mil. 200.
Kipimo cha MRI chenyewe huuzwa kwa USD 400,000 ambazo ni sawa na tsh mil. 840. Na gharama za mafunzo na kuifunga ni tsh. Mil. 300.
Kwa mujibu wa deni wanalotudai hao Phillips la matengenezo tu tungeweza kununua mashine mbili za mri na ct scanner tatu.
Tarehe 20 october kabla ya uchaguzi aliyekua raisi wetu alipokea magari mapya ya washawasha 399, ambayo ni miongoni mwa magari 777 ambayo serikali imeyaagiza kwa ajili ya uchaguzi, ambayo hayakutumika hata magari 50. Hapa ndio pakujiuliza magari yote 777 yalikuwa ma umuhimu gani!
Kwa mujibu wa mtandao wa alibaba, gari moja la washawasha(Riot control vehicle) lenye uwezo wa kubeba little 11500 za cinamon water(maji ya kuwasha), linauzwa kwa USD 250,000 - 400,000. Ambazo ni sawa na tsh mil 500 - 800!
Kwa maana hiyo gari ya washawasha moja na mashine ya mri moja bei hazitofautiani. Kwa maana hiyo yangepunguzwa magari 50 tu, serikali ingeweza kuzifunga mashine za mri na ct scanner katika hospitali zote za mikoa.
Hii inaonyesha serikalini kuna hela, tatizo ni vipaumbele vyetu ambavyo ni vibovu. Chekecha bongo ujue ni kwanini gari la washawasha ni bora kuliko vipimo muhimu kama hivi!

No comments:

ENGEZA HAMU YA CHAKULA MAMII PILI PILI

Zipo katika ubora wa 100% nitamu na yenye laza nzuri