Mkurugenzi wa
Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke
(Kulia)akitoa taarifa ya Pato la Taifa kwa kipindi cha robo tatu ya
mwaka 2014 leo jiji Dar es salaam. Pato hilo kwa mwaka 2014 limefikia
kiasi shilingi trilioni 21.2 kutoka trilioni 19.8 za mwaka 2013,
Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Gregory Milinga,
Aron Msigwa –MAELEZO.
Pato la Taifa (GDP) katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2014 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 21.2 kutoka shilingi trilioni 19.8 za kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jiji Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za
Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke, amesema
kuwa katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 sekta nyingi za uchumi
zimefanya vizuri katika uzalishaji ikilinganishwa na mwaka 2013.
Amesema katika
kipindi hicho shughuli za uchimbaji wa Madini , Mawe na Kokoto zimekua
kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 3.3 za mwaka 2013,
Uzalishaji wa bidhaa za viwandani ukikua kwa asilimia 10.8 kutoka
asilimia 10.4 pamoja na ongezeko la uzalishaji wa umeme kwa asilimia
10.7 kutoka asilimia 10.3 za mwaka 2013 kutokana na matumizi ya mafuta
na Gesi.
Amezitaja sekta
nyingine kuwa ni usambazaji maji ambao umekua kwa asilimia 12.7 kutoka
6.9 za mwaka 2013, Habari na Mawasiliano kwa asilimia 11.9 kutoka 7.0,
Shughuli za Fedha na Bima zikikua hadi kufikia asilimia 13.9 kutoka
asilimia 6.8 za mwaka 2013.
Ameongeza kuwa katika
kipindi hicho huduma za upangishaji wa nyumba zilikua hadi kufikia
asilimia 2.2 kutoka 2.1, shughuli za kitaalamu, kisayansi, ufundi na
utawala zikifikia asilimia 5.4 kutoka asilimia 1.0 ya mwaka 2013.
Bw. Oyuke
amezitaja shughuli nyingine kuwa ni uendeshaji wa Serikali ambazo
zilikua kwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na 4.4, huduma za Elimu kwa
asilimia 3.7 kutoka 3.5, Afya kwa asilimia 8.1 pamoja na shughuli za
Sanaa na Michezo ambazo zilikua kwa asilimia 2.5 ikilinganishwa na 1.6
ya mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment